Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zama za kidijitali lazima zihakikishe manufaa kwa wote: UNCTAD

Zama za kidijitali lazima zihakikishe manufaa kwa wote: UNCTAD

Matumizi ya kidijitali yanaathiri kila upande wa uzalishaji na biashara , kuanzia katika makampuni makubwa hadi kwa wafanyabiashara wadogowadogo, lakini kuna hatari kwamba zama hizi zikaongeza pengo na kutokuwepo usawa wa kiuchumi.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya uchumi ya mwaka 2017 ya kamati ya kimataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD iitwayo "matumizi ya kidijitali, biashara na maendeleo 2017".

Ripoti hiyo inasema teknolojia ya habari na mawasiliano (teknohama), biashara mtandaoni na matumizi ya zana zingine za kidijitali vimewasaidia sana wafanyabiashara wadogo wadogo na wajasiriamali katika nchi zinazoendelea kupata masoko ya kimataifa na kufungua njia zingine za kujipatia kipato.

Miongoni mwa mafanikio hayo inasema ripoti ni kuchagiza uwezeshaji wa wanawake kama wajasiriamali na wafanyabiashara na pia kusaidia katika uzalishaji.

Pia ripoti hiyo imesema uchumi kupitia njia ya kidijitali unakuwa kwa kasi kwenye nchi zinazoendelea ukiongozwa na Uchina na India ambapo asilimia 90 zawa na watu milioni 750 waliingia mtandaoni kwa mara ya kwanza kati ya 2012 na 2015. Katibu mkuu wa UNCTAD ni Mukhisa Kituyi akisema UNCTAD imehamasishwa na uwezo wa mabadiliko ya kidijitali, lakini ni lazima kutambua kwamba mtandao wa inteneti sio tiba kwa maradhi yote.

(SAUTI YA MUKHISA)

"Habari hizi njema za kupanua wigo pia zinakuja na changamoto na hatari zake, kitu kimoja kikubwa kwetu ni kwamba waifaidikaji wakubwa ni wale ambao tayari wana ujuzi na wamejiwekea fursa za kuboresha soko lao, mfano mmoja wa hili ni ukweli kwamba makampuni makubwa manne duniani ndio waongozaji wakubwa katika uchumi wa kidijitali Apple, Alphabet, Microsoft na Amazon."

Na kwa hivyo

(SAUTI YA MUKHISA2)

"Hivyo ni lazima tudhibiti kupanuka kwa pengo  la kutokuwepo usawa baina na nchi na baina ya watu ndani ya nchi kwa ajili ya athari  zilizopo katika mazingira ya sasa."