Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waahidi misaada baada ya kuzuru jimbo la Rhakine

UM waahidi misaada baada ya kuzuru jimbo la Rhakine

Umoja wa Mataifa umeishukuru Serikali ya Myanmar kwa mwaliko wa kushiriki katika ziara  ya kukagua maeneo ya kaskazini mwa Rakhine, ziara  iliyoandaliwa na serikali kwa ajili ya jumuiya ya kidiplomasia na ujumbe Umoja wa Mataifa.

Wawakilishi watatu wa Umoja wa Mataifa walioshiriki  ziara hiyo ni pamoja na Mratibu wa Makazi wa Umoja wa Mataifa Renata Lok-Dessallien; Mwakilishi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, naibu mratibu wa misaada ya Kibinadamu Domenico Scalpelli, na afisa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi  UNHCR Bibi Cécile Fradot.

Ujumbe huo wa Umoja wa mataifa umesema ziara ilikuwa hatua nzuri katika juhudi za kuchunguza maeneo ambayo Umoja wa Mataifa  unaweza kushirikiana na mamlaka ya Myanmar katika kupunguza madhila yanayowakabili watu uko kaskazini mwa Rakhine.

Pia Umoja wa Mataifa umesema, uko tayari kutoa msaada  kwa serikali husika katika kukabiliana na mgogoro wa haki za binadamu katika jimbo hilo, pamoja na utekelezaji wa mapendekezo ya tume ya ushauri ya jimbo la Rakhine