Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matunda ya mradi wa maji Darfur ni dhahiri kwa wakaazi

Matunda ya mradi wa maji Darfur ni dhahiri kwa wakaazi

Eneo la Darfur  nchini Sudan kwa muda mrefu limekabiliwa na ukame wa mara kwa mara ambao husababisha uhasama katika jamii kwa ajili ya kupigania raslimali mbali mbali. Athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri katika eneo hilo ambalo linakabiliana na changamoto mseto ikiwemo mizozo.

Ni kwa muktadha huo ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira, UNEP na wadau wengine kwa ushirikiano na serikali ya jimbo la Darfur Kaskazini na Shirika la Practical Action, Sudan wameanzisha mradi wa kusimamia raslimali asilia kama mbinu ya kuimarisha maisha ya wakazi na kuchagiza amani.

Mradi kwa jina Wadi El Ku Catchment Management Project ambao unafadhiliwa na Muungano wa Ulaya unalenga kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wote kwa njia endelevu. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii upande undani wake.