Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makazi bora kwa kila mtu- UM

Makazi bora kwa kila mtu- UM

Leo ni siku ya makazi duniani ambapo Umoja wa Mataifa unatumia kauli mbiu Sera za makazi:Nyumba kwa gharama nafuu ili kuhakikisha kila mkazi wa dunia ana makazi bora na salama. 

Kupitia siku hii Umoja wa Mataifa unatoa changamoto kwa serikali na watu  kutafakari juu ya hali ya usalama mijini na haki ya msingi ya wote kwa makazi ya kutosha.

Halikadhalika siku hii inakumbusha dunia kwamba kila mtu ana uwezo na wajibu wa kuhahaikisha analinda miji kwa manufaa ya baadaye.

Ajenda ya mwaka huu inazingatia kukuza ngazi zote za serikali na wadau  husika  katika kutafakari jinsi ya kutekeleza mipango thabiti ili kuhakikisha makazi ya kutosha na ya gharama nafuu  kwa wote .

Siku ya makazi duniani ilianzishwa mwaka 1985 na Baraza Kuu la Umoja wa Matifa kupitia azimio namba 40/202, na iliadhimishwa mara ya kwanza mwaka 1986.