Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kukata mgao wa chakula kwa wakimbizi 420,000 Dadaab na Kakuma nchini Kenya

WFP kukata mgao wa chakula kwa wakimbizi 420,000 Dadaab na Kakuma nchini Kenya

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WPF, litapunguza kwa asilimia 30 mgao wa chakula kwa wakimbizi 420,000 walio kwenye kambi za Daadab na Kakuma nchini Kenya. Selina Jerobon na taarifa kamili

(Taarifa ya Selina)

Uamuzi huo umetangazwa na mwakilishi mkazi wa shirika hilo nchini Kenya Bi Annalisa Conte , akisema wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa rasilimali  na hivyo wanahitaji haraka dola milioni 28.5 ili kufikisha msaada wa chakula kwa wakimbizi kwa miezi sita ijayo.

Amesema kutokana na ukata huo kuanzia mwezi huu, WFP itapunguza mgao wa chakula ilhali posho ya fedha itabaki palepale. Afisa habari na mawasiliano wa WFP Kenya Martin Karimi anafafanua kuhusu mgao huo

(Sauti ya Martin)

Na mgao huo utawaathiri vipi wakimbizi

(Sauti ya Martin)

Aidha, WFP haitatoa unga wenye virutubisho  kwa wakimbizi wote kama hapo  awali isipokuwa itapatia kipaumbele wanawake wajawazito na wanawake wanaonyonyesha watoto kupitia kliniki za afya.