Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zahma ya binadamu inahitaji mshikamano wa kimataifa:Lowcock

Zahma ya binadamu inahitaji mshikamano wa kimataifa:Lowcock

Dunia hivi sasa imeghubikwa na zahma ya kibinadamu huku kukiwa na watu milioni 145 wanaohitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kote ulimwenguni.

Amesema hayo mkuu mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA bwana Mark Lowcock. Akizungumza na UN News ameelezea matarajio yake.

(LOWCOC CUT 1)

“Moja ya vitu ambavyo nataka kufanya kama mratibu wa misaada ya dharura ni kuwa wakili wa watu hao, kusikiliza hadithi zao na kusiwasilisha kwa dunia. Nadhani kikubwa nilichokisikia kutoka kwa viongozi ni kujihusisha na masuala ya kibinadamu na madhila  , na nia ya kutaka kuchukua hatua dhidi ya madhila hayo ya kibinadamu.”

Kuhusu suala la kuwaleta pamoja wadau wa kimataifa katika kukabiliana na tafrani hiyo ya kibinadamu amesema

(LOWCOK CUT 2)

“ Kuna uungwaji mkono mkubwa wa kazi ambazo familia ya umoja wa Mataifa inafanya ikiwemo OCHA  katika suala hili, hivyo tunaweza kuwashirikisha watu wote hao tunaotaka kufanya nao kazi , kwa sababu wana nia na wanajali kuhusu masuala tunayoyafanyia kazi.”