Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usipokuwa tayari kubadilika hakuna awezaye kukubadilisha- Rocky Dawuni

Usipokuwa tayari kubadilika hakuna awezaye kukubadilisha- Rocky Dawuni

Malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs yapo 17 na Umoja wa Mataifa unatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa kila mkazi wa dunia hii anayafahamu na anashiriki kuyatekeleza pale alipo. Viongozi wanapiga mbiu lakini mwitikio kutoka kwa wananchi unahitaji utayari wao. Hii ina maana kwamba wananchi waelewe umuhimu wa SDGs kwenye maisha yao na ndipo wasimame kidete  kuyatekeleza. Ni katika muktadha huo Umoja wa Mataifa kupitia mfuko wake, UN Foundation unatumia wanamuziki kama vile Rocky Dawuni, mwanamuziki kutoka Ghana na pia balozi mwema wa mfuko huo, kuchagiza malengo hayo. Rocky hivi karibuni alifika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New  York, Marekani kutumia sanaa yake kupasha ujumbe. Assumpta Massoi alikutana naye na kuandaa makala hii..