Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa ombi la ufadhili kwa ajili ya wakimbizi wa Burundi

UNHCR yatoa ombi la ufadhili kwa ajili ya wakimbizi wa Burundi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeisihi jamii ya kimataifa isaidie wakimbizi wa Burundi na wenyeji wanaowahifadhi wakati huu ambao ukosefu wa ufadhili unahatarisha juhudi za kuwasililisha misaada ya kibinadamu wanakohifadhiwa wakimbizi.

Kwa mujibu wa UNHCR takriban wakimbizi 420,000 wa Burundi walioko nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC, Rwanda, Uganda na Tanzania wana mahitaji ya dharura.

Kufikia sasa ni asilimia 19 tu ya ufadhili wa ombi la dola milioni 429 umepatikana kwa ajili ya wakimbizi wanaoishi nchi jirani.

Msemaji wa UNHCR Geneva, Andrej Mahecic anasema..

(Sauti ya Mahecic)

“Hii ina maana kwa watu wa mashinani ni muhimu kubadili vipaumbele na kupanga upya mambo mara kwa mara ili kuhakikisha shughuli za kuokoa maisha zinasalia, misaada haitoshi, wakimbizi 88,000 wanaishi makazi yenye paa za plastiki na hiyo ni changamoto kwa watoa huduma.”