Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuyakabili magonjwa ya moyo: WHO

Tuyakabili magonjwa ya moyo: WHO

Ikiwa leo ni siku ya moyo duniani, inayoungwa mkono na shirika la afya ulimwenguni WHO, msisitizo waa siku hii ni kukabiliana na magonjwa ya moyo VCDs, ambayo yanasababisha vifo vya watu milioni 7.7 kila mwaka, ikiwani  asilimia 31 ya vifo vyote ulimwenguni.

Kwa mujibu wa WHO, vichocheo vya magonjwa haya ambayo kimsingi hujidhihirisha kupitia mashambulizi ya moyo na kiharusi, ni matumizi ya tumbaku, ulaji usiozingatia afya, kutofanya mazoezi na matumizi holela ya vilevi.

Magonjwa haya huonekana kwa watu kupitia shinikizo la damu, kuongezeka kwa kiwango cha glukosi damuni, pamoja na utipwatipwa ambavyo huhatarisha afya njema ya moyo.

Akizungumzia magonjwa ya moyo ambayo yako katika kundi la yale yasiyoambukiza NCDs, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk  Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema magonjwa haya yanaathiri zaidi nchi zinazoendelea.

Amesema chanzo cha magonjwa haya yanaweza kuzuilika.

(Sauti Tedro)

‘‘Kupitia sera ambazo zinaimarisha udhibiti wa tumbaku na pombe, kusaidia kuimarisha milo, na ufanyaji mazoezi.’’