Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno la wiki: Likiza

Neno la wiki: Likiza

Wiki hii tunaangazia neno "Likizai" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Je, neno hili lina maana ngapi?

Bwana Sigalla ansema neno Likiza lina maana zaidi ya moja, la kwanza ni kumpa mtoto mchanga ambaye bado ananyonyeshwa chakula kingine mbali na maziwa ya mama ili aanze kuzoea. Ya pili ni kusitisha au kumpumzisha mtu kufanya jambo ambalo amekuwa akifanya