Polisi wanawake wa UNPOL ni wakweli na wakarimu: Busingye

29 Septemba 2017

Ukweli na ukarimu unaodumiswa na polisi wanawake unachangia kwa kiasi kikubwa majukumu ya polisi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNPOL. Hayo ni kwa mujibu wa inspekta wa polisi msaidizi wa UNPOL Kellen Busingye kutoka Rwanda anayetumika katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchuni humo UNMISS.

UNPOL imekuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha raia wanasalia salama. Mjini Juba raia 38,000 wanaishi katika maeneo ya ulinzi wa raia kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa na kama ilivyo katika miji mingine magenge na uhalifu ni changamoto kubwa. Inspekta msaidizi Kellen Businga ambaye ni moja kati ya maafisa wa polisi wanawake 260 kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaotukima na UNMIS ameshiriki operesheni ya kusaka wahalifu na silaha haramu nje ya kambi na anajivunia anachofanya

(KELLEN CUT 1)

“Nahisi vizuri sana kwa matukio hayo kwa sababu niko hapa kwa ajili ya kulinda raia na kuwakinga na madhara, hivyo nahisi kwamba ninatimiza wajibu ulionileta hapa Sudan Kusini.”

Kellen anatoa changamoto wa wanawake wengine wanaohisi kazi ya polisi ni mtihani mgumu

(KELLEN CUT 2)

“Napenda kuwatia moyo kwamba kazi hii ni nzuri, ni vizuri kutumikia taifa na Umoja wa Mataifa. Ninajivunia sana kuiwakilisha nchi yangu kama sehemu ya Umoja wa Mataifa na kusaidia kutekeleza wajibu wa mpango wa kulinda Amani , UNMISS ili kuwalinda raia.”

Amesema kushiriki katika kazi hii kuna matunda yake

(KELLEN CUT 3)

“Faida moja kubwa ni uzoefu kwenye mpango huu, nitautumia uzoefu huo nikirejea nyumbani. Sababu nyingine ni kwamba wasicha ni lazima walitumikie taifa lao, dunia na kuhisi kwamba wana ujasiri wa kufanya hivyo. Hii sio kazi ya wanaume pekee  lakini na wanawake pia na wanaweza kufanya vyema kuliko wanaume.

Kwa sababu

(KELLEN CUT 4)

“wanawake ni wakarimu, ni waaminifu, wanasema ukweli. Ni shupavu, wavumilivu na wanauwezo wa kuhimili hali zote”.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter