Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanaopata misaada Syria sasa imeongezeka- Egeland

Idadi ya wanaopata misaada Syria sasa imeongezeka- Egeland

Idadi ya watu wanaofikishiwa misaada kwenye maeneo yanayoshikiliwa na vikosi vya serikali na wapinzani nchini Syria imeongezeka.

Hiyo ni kwa mujibu wa mshauri maalum wa mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Jan Egeland wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi hii leo baada ya kikao cha

kikosi kazi cha kimataifa cha usaidizi kwa Syria.

(Sauti ya Egeland)

“Hivi sasa tunafikia wasyria kati ya milioni 7 hadi milioni 9 kila mwezi katika moja  ya operesheni kubwa zaidi ya kibinadamu ya kizazi cha sasa.”

Amesema asilimia 95 ya wasyria wako kwenye maeneo yanayoshikiliwa na serikali na asilimia 2 wanaishi kwenye maeneo yaliyo chini ya upinzani ilhali waliosaliwa wako kwenye maeneo  yanayoshikiliwa na pande zote.

Hata hivyo amesema licha ya nuru  hiyo ya kufikia watu wengi bado kuna changamoto..

(Sauti ya Egeland)

“Hatuwezi kulinda raia, hivi karibuni hali imezidi kuwa mbaya katika ulinzi wa raia na wafanyakazi wale wa kutoa misaada.”