Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kichaa cha mbwa chaendelea kupiga kambi Asia na Afrika- WHO

Kichaa cha mbwa chaendelea kupiga kambi Asia na Afrika- WHO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha jamii juu ya athari za ugonjwa wa kichaa cha mbwa, shirika la afya duniani, WHO limesema ugonjwa huo umeendelea kutikisa katika nchi zaidi ya 150 na maeneo licha ya kwamba unazuilika.

Msemaji wa WHO huko Geneva, Uswisi Tarik Jasarevic amesema maeneo yaliyoathirika zaidi ni Asia na Afrika ambapo asilimia 99 ya maambukizi ya ugonjwa huo yanasabishwa na mbwa.

Amesema ugonjwa huo unaweza kutokomezwa kwa mbwa kupatiwa chanjo na kwamba..…

(Sauti ya Tarik)

“Kwa binadamu kuna chanjo kabla ya kung’atwa ambayo hupendekezwa kupatiwa watu ambao mara kwa mara wanakuwa karibu na mbwa ili kuepusha wasiambukizwe kichaa cha mbwa na pia kuna ile inayotolewa baada ya mtu kung’atwa na mbwa. Katika baadhi ya nchi ni aghali sana na ni vigumu kuipata.”

WHO inasema asilimia 40 ya watu wanaong’atwa na Wanyama wanaosababisha kichaa cha mbwa ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 15.