Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama ladadili ugaidi na usalama wa anga

Baraza la usalama ladadili ugaidi na usalama wa anga

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana mjini New york Marekani kujadili vita dhidi ya ugaidi katika usafiri wa anga.

Kikao hicho kilichojumuisha uwakilishi wa shirika la kimataifa la usalama wa anga ICAO na kamati ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi kimepokea ripoti kutoka ICAO na njia za kudumisha ushirikiano baina ya pande hizo mbili ili kupambana na tishio hilo la kimataifa.

Kwa pamoja Dkt.  Fan Liu , Katibu mkuu wa ICAO na balozi Abdellatif Aboulatta ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kupambana na ugaidi wamewasilisha ripoti  kwenye kikao hicho ikelezea hatua zilizopigwa tangu kuanzishwa kwa ICAO yapata miaka 70 iliyopita .

Dkt. Fan amesema kikubwa zaidi ni ushirikiano uliopo miongoni mwa nchi wanachama katika kuukabili ugaidi na kubadilishana taaluma na pia taarifa za kimtandao na mashirika ya ulinzi na serikali mbalimbali.

Hata hivyo amesema kuna changamoto wanaozokabiliana  nazo hasa katika katika kubadilishana tarifa kwa kutumia teknolojia na hii ni kwa nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea.

(Sauti ya Dkt. Fan)

Ni kwamba ushirikiano baina ya nchi mbalimbali katika hilo unasuasua . Lazima tutafute jinsi ya kufikia muafaka katika kubadilishana taarifa muhimu katika kiwango stahiki. Azimio namba 209 linatilia mkazo jambo hili na baadhi ya nchi washirika pamoja na sisi tumekubaliana katika kufikia muafaka.”