Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yataka juhudi za kimataifa kuimarisha ajira kwa vijana Afrika Kaskazini

ILO yataka juhudi za kimataifa kuimarisha ajira kwa vijana Afrika Kaskazini

Wakati viwango vya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana katika nchi za Afrika Kaskazini ni asilimia 28.8, ikiwa ni mara mbili ya kiwango kimataifa, shirika la kazi duniani limetaka nchi hizo kuchukua hatua zaidi kukabiliana na janga hilo.

Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na ILO huko Geneva, Uswisi lenye kaulimbiu “Imarisha vitendo kwa ajili ya ajira kwa vijana,” Naibu Mkurugenzi wa sera, ILO Deborah Greenfield amesema kuziba hilo pengo la ajira kunahitaji ushirikiano baina ya jamii, serikali, mashirika ya wafanyakazi na waajiri pamoja na wadau wa maendeleo.

Bi. Greenfield amesema sera thabiti zinahitajika ili kukabiliana na hali ya sasa.

Afrika Kaskazini inakabiliwa na ukosefu wa ajira kwa vijana na ushiriki mdogo katika masuala ya kiuchumi ambapo ni asilimia 16.6 ya vijana wa kike na asilimia 46.8 ya vijana wa kiume ndio wanashiriki kwenye uchumi wakiwa pengine wameajiriwa au wanasaka ajira.