Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza Saudi Arabia kwa kuruhusu wanawake kuwa madereva

UM wapongeza Saudi Arabia kwa kuruhusu wanawake kuwa madereva

Hatimaye nchi pekee duniani iliyokuwa inazuia wanawake kuendesha magari imeondoa zuio hilo, hatua iliyopokewa kwa shangwe na pongezi kona mbali mbali za dunia. Selina Jerobon na taarifa kamili.

(Taarifa ya Selina)

Nats…

Huyu ni Mwakilishi wa kudumu wa Saudi Arabia kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Abdallah Al-Mouallimi akiwaeleza wajumbe waliokutana kwa kikao cha Baraza la Usalama kuwa bila shaka wangalipenda kufahamu kuhusu amri  ya kifalme iliyopitishwa nchini mwake ya kuwapatia wanawake haki ya kuendesha gari..

(Sfx)+ (Sauti ya Balozi Abdallah)

“Hii ni siku ya kihistoria kwa jamii ya Saudia kwa wanawake na wanaume. Tunaweza sasa kusema.. hatimaye.”

Naye Katibu Mkuu António Guterres kupitia ukurasa wake wa Twitter amekaribisha hatua ya mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud kutoa agizo la kuondoa zuio hilo akisema ni hatua muhimu kwenye mwelekeo wa haki.

Idhaa ya Umoja wa Mataifa ilizungumza na Mohammad Naciri ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake UN Women katika nchi za kiarabu ili kupata maoni yake kuhusu hatua hiyo..

(Sauti ya Mohammad)

“Tunaona kama hatua ya kiashiria kutoka kwa ufalme wa Saudi Arabia kuelekea kwenye fursa zaidi ya haki kwa wanawake wa Saudia kwenye ufalme huu.”

image
Picha: Kwa ruhusa ya Wizara ya mambo ya nje ya Saudi. (UM file #281510)
Amesema kwa wanawake nchini Saudi Arabia uamuzi huo ni mwendelezo wa hatua muhimu ambazo zimekuwa zikichukuliwa na ufalme wa nchi hiyo….

(Sauti ya Mohammad)

“Kwa kuteua wanawake wa Saudi katika bunge la Saudia au baraza la Shura na pia kupitisha sheria kuhusu ukatili wa kingono na hatua hii ya lengo inafungua milango zaidi kuelekea usawa kwa masuala ya wanawake.”