Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawasaidia watu wapya wanaotawanywa Hawija Iraq

IOM yawasaidia watu wapya wanaotawanywa Hawija Iraq

Watu zaidi ya 2400 wametawanywa kwenye mji wa Hawija jimbo la Kirkuk na majimbo ya  Shirqat na salah al-Din, katika operesheni ya kijeshi ya kutaka kuikomboa wilaya ya Hawija.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM watu hao walioanza kutawanywa tangu septemba 21 wengi wao wanakimbilia katika jimbo la Ninewa wakiwemo watu 1700 ambao wamesafirishwa kwa mabasi na uongozi wa Iraq hadi kwenye kituo cha dharura cha IOM cha Haj al kilichopo kilometa 60 Kusini mwa mji wa Mosoul.

Idadi kubwa ya wakimbizi hao wa ndani wanaowasili Haj Ali ni watoto, wanawake na wazee, na IOM inasema wakati operesheni inaendelea wanategemea maelfu ya familia zitatawanywa na kuhitaji msaada wa kibinadamu.