Nilikuwa muathirika wa FGM lakini sasa mimi ni mshindi- Inna Modja

22 Septemba 2017

Ukatili wa aina yeyote dhidi ya wanawake na wasichana hauna nafasi katika dunia hivi sasa kwani unakwamisha mendeleo. Yaelezwa kuwa ili kukabiliana na ukatili huo ni lazima kufahamu sura ambazo unachukua ili kuweza kukabiliana nao.

Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii ambapo mwanamuziki Inna Modja kutoka Mali anatuma ujumbe kutumia muziki akisema kwamba yeye binafsi aliwahi kuwa muathirkia wa ukatili dhidi ya wanawake.