Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utesaji wa washukiwa ni kinyume cha maadili, sheria na hauna ufanisi:Zeid

Utesaji wa washukiwa ni kinyume cha maadili, sheria na hauna ufanisi:Zeid

Utesaji wakati wa kuhoji washukiwa wa makossa mbalimbali ni ukiukaji wa sheria za haki za kimataifa, ukiukaji wa maadili na ni mbinu isiyo na ufanisi.

Hayo yamesemwa leo na Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’aad al-Hussein katika kikao maalumu kuhusua suala la utesaji kilichofanyika kandoni mwa mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Katika mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya haki za binadamu Zeid amesema njia za utesaji huwanfanya watu mara nyingi kukiri makosa ambayo hawajafanya na njia zingine huenda mbali zaidi hata kusababisha washukiwa kupoteza maisha. Akioanisha na usemi wa Napoleon wa mwaka 1796 amesema

(SAUTI YA ZEID)

“Utesaji wa mahabusu ambao wamekamatwa na hawawezi kujitetea unaleta gadhabu kwa jamii zao na kuchagiza hamasa ya kulipiza kisasi, utesaji unaweza kukuza wigo wa chuki na ghasia zaidi”.

Licha ya ukweli huo amesema bado kuna nchi nyingi ambazo ukikamatwa una nafasi kubwa ya kupigwa, kunyanyaswa na kuteswa na washukiwa wengi hawapewi fursa ya kuwakilishwa kisheria au kufikishwa mbele ya jaji. Na nchi zingine amesema zimekwenda mbali zaidi hata kutumia

(SAUTI YA ZEID)

Njia za kikatili za kuwahoji washukiwa kama kuwazamisha kwenye maji, kuwalazimisha mahabusu kuingia katika makontena madogo, kuwashurutisha kukaa mkao wa aina moja unaowaumiza kwa muda mrefu, au kuwabamiza ukutani. Na zaidi ya hayo mara nyingi hali ya mahabusu ni mbaya isiyokidhi viwango, ikiambatana na unyanyasaji wa hali ya juu ulio kinyume na mkataba wa kupinga utesaji, na hii ni kweli hata katika  nchi nyingi zilizoendelea.”

Amesisitiza hali hii haipaswi kufanywa na posili au mifumo ya sheria popote pale duniani, kwani maafisa wanaosisitizautekelezaji wa sheria hawapaswi kuivunja.