Neno la wiki: Utengamano na Utengano

22 Septemba 2017

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Utengamano" na "Utengano".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema utengamano ni hali kuwa kwa pamojan au kushirikiana, na utengano ni kinyume cha utengamano, yaani hali ya kutokuwepo pamoja, iwe kimawazo au kiuhalisia...