Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 15 tu ndizo zenye sera tatu muhimu kwa ajili ya malezi ya watoto-UNICEF

Nchi 15 tu ndizo zenye sera tatu muhimu kwa ajili ya malezi ya watoto-UNICEF

Ni nchi 15 tu kote duniani ambazo zimeweka sera za kimsingi kitaifa kuwezesha wazazi,  raslimali na muda unaohitajika kwa ajili ya malezi ya watoto ili kuhakikisha ubongo wao unanakua na afya inayostahili kwa ajili ya ukuaji na mustakhbali wao, imesema ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Flora Nducha na tarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNICEF iliyozinduliwa leo nchi 32 ambako wananaishi mtoto mmoja kati ya wanane mwenye umri wa chini ya miaka mitano hazina sera hizo kabisa.

Ripoti imesema kwamba siku za awali katika maisha ya kila mtoto ni muhimu, miaka miwili ya elimu ya bure ya awali, likizo zenye malipo katika miezi sita ya kwanza ya maisha ya mtoto , miezi sita ya likizo kwa mama anapojifunugua  na baba wiki nne za likizo kwa ajili ya kuwezesha kumjengea msingi thabiti wa malezi mtoto.

UNICEF imesema sera hizi zinawasaidia wazazi kulinda watoto na kuwapatia lishe bora, kucheza nao na elimu katika miaka ya kwanza ya maisha ya mtoto wakati ubongo wao unakua katika kasi ya kipekee.

Cuba, Ufaransa, Ureno, Urusi na Uswizi ni miongoni mwa nchi ambazo kuna sera hizi tatu muhimu lakini watoto milioni 85 wa umri wa  chini ya miaka mitano wanaishi katika nchi 32 ambako hakuna sera hizo wakati asilimia 40 ya watoto hawa wanaishi katika nchi mbili ikiwemo Bangladesh na Marekani.