Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto na barubaru milioni 617 hawana ujuzi wa kusoma na hisabati:UNESCO

Watoto na barubaru milioni 617 hawana ujuzi wa kusoma na hisabati:UNESCO

Twakimu mpya kutoka taasisi ya data ya shirika la Umoja wa mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO (UIS) zinaonyesha kwamba watoto na barubaru milioni 617 kote duniani hawafikii kiwango cha chini cha ujuzi katika kusoma na hisabati.

Kwa mujibu wa UIS hiyo ni ishara ya mtafaruku katika elimu ambao unaweza kutishia hatua zilizopigwa katika kufikia ajenda ya Umoja wa Mataifa ya malengo ya maendeleo endelevu SDG’s hususani lengo namba 4.

Takwimu hizo zilizotolewa leo zinaonesha kwamba watoto zaidi ya milioni 387 wa shule za msingi  au asilimia 56 na barubari milioni 230 wa shule za sekondari au asilimia 61 hawatofikia kiwango cha chini cha ujuzi wa kusoma na hisabati.

Nchi za Afrika Kusini kwa jangwa la Sahara zikitajwa kuwa waathirika wakubwa  ambako watoto na barubaru milioni 202 hawasomi masomo hayo muhimu na karibu watoto 9 kati ya 10 wa umri wa kati ya miaka 6 na 14 hawatofikia kiwango cha chini cha ujuzi wa kusoma na hisabati.

Nchi za Asia ya Kati na Kuisni zimeelezwa kushika nafasi ya pili zikiwa na asilimia 81 au watoto na barubaru milioni 241 wasiosoma.