Kusaidia wakimbizi na wahamiaji sio wajibu ni mshikamano:Guterres

20 Septemba 2017

Mwaka mmoja tangu kupitishwa kwa kauli moja azimio la New York kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji bado kuna changamoto kubwa katika suala hilo ingawa pia matumaini yapo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres kwenye mkutano maalumu kuhusu wakimbizi na wahamiaji uliofanyika leo kandoni na kikao cha baraza kuu kinachoendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Guterres amesema azimio hilo lililopitishwa ni thibitisho imara lililofungua njia ya kusaka suluhu ya kudumua ya matatizo yanayowakabili wakimbizi na wahamiaji, akisistiza kuwa kuwasaidia sio wajibu bali ni kuonyesha mshikamano kwa madhila wanayopitia.

Ameongeza kuwa ingawa kuna hatua ambazo zimeanza kupuigwa lakini vado sio kila mahali awakimbizi na wahamiaji wanakubalika , hivyo amependekeza mambo matano ya kuyatilia maanani kuanzia mwakani

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres . Picha: UM/Evan Schneider

(SAUTI YA GUTERRES)“Mosi ni kufufua mpango wa kuleta tena uaminifu katika mpango wa ulinzi kwa wakimbizi, pili tunahitaji kuanzisha mkakati wa ushirikiano wa kitaifa na kimataifa unakaojumuisha suala la watu kuhama, tatu tunahitaji uwajibikaji kwa wasafirishaji haramu wa binadamu wanaofaidika kwa kuwatumia watu hawa wasiojiweza, nne hatutaweza kumaliza majanga tunayoyaona kwenye baharí ya mediterrania, Ghuba ya Aden na sehemu zingine duniani bila kuanzisha fursa zaidi kwa wahamiaji wa mara kwa mara na wa halali na kwa kushirikiana vyema”

Na tano na mwisho  Katibu Mkuu amesema dunia inakabiliwa na changamoto kubwa ya mabadiliko katika soko la ajira, hivyo ni lazima kufikiria kwa kina athari za upungufu wa wafanyakazi wenye utaalamu , kwa sababu hiyo amesema mkakati wowote mpya kuhusu wahamiaji ni lazima ulijumuishe suala hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter