Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaochagiza machafuko Sudan Kusini lazima wawajibishwe

Wanaochagiza machafuko Sudan Kusini lazima wawajibishwe

Wito umetolewa leo na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuhakikisha kwamba wanaochochea machafuko ya Sudan kusini wanawajibishwa lakini pia misaada ya kibinadamu inawafikia walenga. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GRACE)

Wito huo umetolewa kwenye mkutano maalumu kuhusua hali ya kibinadamu na usaidizi Sudan kusini ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA na kushirikisha wadau mbalimbali wa kimataifa ukiwemo Muungano wa Afrika, Muungano wa Ulaya, na mashirika ya kimataifa ya misaada .

Wadau hao wametoa dukuduku zao kuhusu hali inayoendelea Sudan Kusini na nini kifanyike Miongoni mwao ni Bi Sessouma Minata Samate Kamishina wa Muungano wa Afrika kuhusu masuala ya kisiasa akisisitiza kuvunjika kwa chungu sio mwisho wa kupika.

(SAMATE CUT)

Kushughulikia hali ya kibinadamu na kuunga mkono mchakato wa amani katika nchi hiyo ni jukumu letu sote kuchukua hatua katika hali ya dharura na kusaidia juhudi za serikali ya Sudan kusini

Naye kamishina wa Muungano wa Ulaya wa misaada ya kibinamu Christos Stylianedes ameonya dhidi ya wanaochochea machafuko Sudan Kusini

(STYLIANEDES CUT)

Hatutonyamaza na tusikae kimya tukaliangalia taifa hili likisambaratika, waharibifu lazima waambie bayana kwamba watawajibishwa kwa vitendo vyao, tutaunga mkono juhudi za Umoja wa mataifa kuiwajibisha serikali.”