Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujikita na watu, amani na usalama ndio ajenda yetu Uganda:Museveni

Kujikita na watu, amani na usalama ndio ajenda yetu Uganda:Museveni

[caption id="attachment_327225" align="aligncenter" width="625"]overnightmuseveni

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesema kauli mbiu ya mjadala wa baraza kuu mwaka huu, kujikita na masuala ya watu, amani, usalama na mustakhbali bora kwa wote ni muafaka kwa sasa na ndio ajenda ya Uganda pia ikizingatia kwamba dunia imeghubikwa na machafuko, na majanga ya asili.

Akihutubia katika mjadala huo wa wazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani amesema dunia ina mengi ya kufaidika nayo ikiwa mahala bora pa kuishi,  akihoji nani atakayepoteza chochote endapo dunia itakuwa na amani, usalama, bila ugaidi, bila njaa , mazingira bora, maji ya kutosha na afya bora.?

Rais Museveni ambaye amesema amekuja na mwaswali mengi kuliko majibu kwenye mjadala wa mwaka huu hakulisahau swali kuhusu mustakhbali wa nyuklia ya Jamhuri ya watu wa Korea au DPRK na uhusiano wake na jirani zao Korea Kusini

(Sauti ya Museveni )

“Ni nani atakayepoteza chochote endapo Korea Kaskazini na Korea Kusini wataachwa wajadili muungano wao? ni watu wamoja, badala ya kuwa na mgawanyiko katika rasi hiyo, na ni kazi yetu kuudhibiti mgawanyiko huo bila kuchoka.”

Na baada ya hotuba hiyo Rais Museveni alizungumza na idhaa hii kuhusu wakimbizi wa Sudani Kusini wanaoendelea kuingia Uganda akisema..

(Sauti ya Museveni)