Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani vikali mashambuli ya Houthi dhidi ya raia Yemen

UM walaani vikali mashambuli ya Houthi dhidi ya raia Yemen

Kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya raia nchini Yeemen, tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani mashambulizi hayo yanayotekelezwa na vikundi washirika vya Houthi, na vikosi vya wanajeshi walio watiifu kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Ali Abdullah Saleh, pamoja na muungano wa wapiganaji unaoongozwa na Saudia.

Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Rupert Colville, wamethibitisha kuwa watoto watatu waliuauwa na wengine saba walijeruhiwa, katika mashambulio ya wapiganaji wa Houthi, mjini Taiz wilayani Salah, katika siku tano zilizopita.

Watu wengine 12 wakiwemo watoto watano waliuauwa katika shambulio la anagni kule Marib. Bwana Covile ameongeza kuwa, wafuatiliaji wao wameripoti kwamba watoto wote waliouauwa au kujeruhiwa walikuwa wa umri kati ya miaka sita hadi 13.

Akihutubia wiki jana, Kamishina Mkuu wa haki za binadamu alisema, jumla ya raia 5,159 waliuauwa na wengine 8,761 wamejeruhiwa tangu Machi 2015.