Tishio la nyuklia,ujumbe thabiti uonane na Rais wa DPRK- Buhari

Tishio la nyuklia,ujumbe thabiti uonane na Rais wa DPRK- Buhari

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amehutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa #UNGA72 akisema kuwa kitisho kikubwa hivi sasa duniani ni nyuklia.

Amesema tangu janga la kombora la Cuba mwaka 1962, dunia haijawahi kuwa karibu zaidi na kukumbwa na vita vya nyuklia kama ilivyo sasa kutokana na majaribio ya silaha za nyuklia yanayofanywa na Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK au Korea Kaskazini.

Rais Buhari amewaambiwa viongozi wa nchi wanachama kuwa ni lazima juhudi za kidiplomasia zifanyike ili kusuluhisha mgogoro huo unaotishia usalama wa kimataifa akisema.. 

“Nigeria inapendekeza ujumbe thabiti wa Umoja wa Mataifa uanze mazungumzo ya haraka na kina na kiongozi wa Korea Kaskazini. Ujumbe huo ukiongozwa na Baraza la Usalama, unapaswa kujumuisha wajumbe kutoka kanda zote.”