Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pengo la ujira ni ubaguzi na lazima ukomeshwe: UN Women

Pengo la usawa katika malipo baina ya wanawake na wanaume ni ubaguzi ambao unapaswa kupatiwa dawa mujarabu.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women,  Phumzile Mlambo Nguca katika mjadala maalumu kwenye baraza Kuu hii leo uliojikita katika hatua za Umoja wa Mataifa katika kusala suluhu ya kuziba pengo la ujira.

Bi Nguca amesema suala hilo ni muhimu kwa UN Women kwa sababu , ni mfumo mwingine wa ubaguzi dhidi ya wanawake ambao umekuwa ukifumbiwa macho kwa muda mrefu.

Ametaja kuwa wanawake wengi duniani hawathaminiwi inavyostahili  sanjari na kazi wanazofanya, na haijalishi kama wako katika ngazi ya juu ya uongozi aun dio kwanza waana anza kazi. Kwa kulitambua hilo amesisitiza ndio maana malengo ya maendeleo endelevu SDG’s yamedhamiria kutokomeza mifumo yote ya ubaguzi dhidi ya wanawake.

Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa mashirika, pia asasi za kiraia kushikamana katika kushughulikia suala la usawa katika malipo na mifumo mingine ya ubaguzi dhidi ya waanwake ili kizazi kijacho kisipitie machungu wanayopitia wanawake wa kizazi hiki na kabla ya kuchelewa zaidi na ubaguzi huo ukageuka kuwa sheria.

Pengo la ujira ni ubaguzi na lazima ukomeshwe: UN Women

Pengo la usawa katika malipo baina ya wanawake na wanaume ni ubaguzi ambao unapaswa kupatiwa dawa mujarabu.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women,  Phumzile Mlambo Ngcuka katika mjadala maalumu kwenye baraza Kuu hii leo uliojikita katika hatua za Umoja wa Mataifa katika kusala suluhu ya kuziba pengo la ujira.

Bi Ngcuka amesema suala hilo ni muhimu kwa UN Women kwa sababu , ni mfumo mwingine wa ubaguzi dhidi ya wanawake ambao umekuwa ukifumbiwa macho kwa muda mrefu.