Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia sasa iko vipande vipande- Guterres

Dunia sasa iko vipande vipande- Guterres

Mjadala wa wazi wa kikao cha 72 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani Katibu Mkuu António Guterres akisema dunia hivi sasa imemeguka vipande vipande badala ya kuwa na amani. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Nats..

Kiashiria hicho cha kuanza kwa kikao, mjadala wa wazi, Rais wa Baraza Kuu Miroslav Lajčák akikaribisha wajumbe…

Nats…

Na ndipo mtendaji mkuu wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu António  Guterres akawasilisha ripoti yake ya mwaka kuhusu kazi za Umoja huo.

Ripoti hiyo pamoja na kueleza kile ambacho kimetekeleza, imeangazia kwa kiasi kikubwa imeangazia madhila yanayokumba duniani hivi sasa kuanzia tishio la nyuklia, ugaidi, mabadiliko ya tabianchi, vita na mizozo akisema..

image
Moja ya nukuu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo. (Picha:UNSocialMedia)
(Sauti ya Guterres-1)

“Tuko na dunia iliyo vipande vipande. Tunatakiwa kuwa dunia yenye amani. Na ninaamini kuwa pamoja tunaweza kujenga amani, tunaweza kurejesha imani na kujenga dunia bora kwa wote.”

Kwa Myanmar akasisitiza wakomeshe mashambulizi ya kijeshi dhidi ya warohingya huku ugaidi akisema muarobaini ni kumaliza vyanzo vya mizozo hiyo na zaidi ya yote ni janga la wakimbizi na wahamiaji akisema…

(Sauti ya Guterres-2)

“Wakimbizi wa ndani si tatizo. Tatizo ni mizozo, mateso na ufukara.”

Baada ya Guterres Rais wa Baraza Kuu Bwana Lajčák akasema zungumza na kutoa wito kwa marais na viongozi hao akisema…

(Sauti ya Lajčák)

“Hatuwezi kushindwa! Na tukishidwa tunaweza kusema kuwa Umoja wa Mataifa ndio jukwaa bora la kutatua changamoto za dunia. Wale wanaoubeza wataonekana wako sahihi, na wengine washindwa kuwa na matumaini.”

Kwa mara ya kwanza Rais Donald Trump wa Marekani alipanda jukwaani kuhutubia Baraza hilo akisisitiza ajenda yake ya marekebisho ya Umoja wa Mataifa akisema gharama ni kubwa na Marekani inachangia kiwango kikubwa.

(Sauti ya Trump)

“Lakini iwapo unaweza kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwake hususan lengo  la amani, uwekezaji  huu ungalikaribishwa kwa urahisi.”