Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili ni kiini cha ufanikishaji wa agenda ya 2030: Guterres

Ufadhili ni kiini cha ufanikishaji wa agenda ya 2030: Guterres

Watu wengi duniani wamesalia katika umasikini uliokithiri, na hali isiyokubalika ya kutokuwepo kwa usawa inaendelea. Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano wa ngazi ya juu wa ufadhili wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu unafanyika hapa kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa New york.

Guterres amesema inatambulika kwamba utandawazi umeleta faida kubwa , lakini pia ni bayana kwamba hauko sawia na sio endelevu.

Ameongeza kuwa pengo kubwa linaonekana katika umuhimu wa utandawazi , lakini

(SAUTI YA GUTERRES)

Ajenda ya 2030 na malengo ya maendeleo endelevu ni mpango wa kudumisha na kujenga utandawazi wa haki na endelevu na kukabiliana na upinzani ambao bado upo katika maeneo mengi duniani na ufadhili ni muhimu sana katika kutimiza hilo .”

Amesema anaamini dunia ina rasilimali za kutosha kutimiza ajenda ya 2030 cha msingi ni kuhakikisha zinapelekwa kunakohitajika zaidi kwani ufadhjili unahitaji juhudi za muda mrefu na kwamba

(SAUTI YA GUTERRES)

Uchaguzi tutakaofanya katika ufadhili utakuwa muhimu sana .Tunaweza kuchagua kukumbatia ukosefu wa fedha kwa ajenda ya 2030 katika ulimwengu unaoishi na fedha nyingi zinazofadhili masuala yasiyo na maana na faida au tunaweza kuchukua fursa ya ya kuelekeza ufadhili  huo kulingana na mahitaji yetu ya haraka, na ya pamoja. Uchaguzi unaonekana bayana, hebu tuwekeze katika ajennda ya 2030 na tufadhili wa ulimwengu bora kwa wote.