IOM yaomba dola zaidi ya milioni 4 kusaidia waathirika wa vimbunga Irma na Jose

18 Septemba 2017

Mapema mwezi huu vimbunga Irma na Jose vilipiga na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa katika visiwa vya Caribbean, ukanda wa Bahamas, Cuba na Marekani.

Leo shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limetoa ombi la dola milioni 4.95 kwa jumuiya ya kimataifa ili kuzisaidia haraka jamii  hizo zilizoathirika katika ujenzi mpya.

Fedha hizo zitalisaidia shirika la IOM kupeleka msaada wa wataalamu wa masuala ya kiufundi na pia makundi miongoni mwa jamii hizo kuweza kufikisha msaada wa kibinadamu , kusimamia uhamishaji wa watu, kuhakikisha uwajibikaji na kuwezesha ujenzi mpya wa jamii hizo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter