Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa yakaribisha uchaguzi wa rais mpya wa HirShabelle Somalia

Jumuiya ya kimataifa yakaribisha uchaguzi wa rais mpya wa HirShabelle Somalia

Umoja wa Mataifa , Muungano wa Afrika, Muungano wa Ulaya , IGAD, Ethiopia, Italia, Sweden, Uingereza na Maekani wamempongeza Mohamed Abdi Ware kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa HirShabelle katika kura iliyopigwa kwenye bunge la jimbo laHirShabelle jana.

Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM upigaji kura ulifanyika katika mpangilio ,mchakato wa uwazi na wa hadharani.

Katika taarifa yao ya pamoja washirika hao wa kimataifa wamekaribisha kukamilika kwa uchaguzi huo kwa njia iliyopangwa na kuzingatia mchakato wa sheria.

Pia wameendelea kuzitaka pande zote kuheshimu matokeo ya kura hiyo ya bunge la kikanda na kujizuia na hatua zozote ambazo zitaathiri mchakato wa ujenzi mpya wa taifa hilo.