Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita na mabadiliko ya tabianchi yaongeza njaa duniani:UM

Vita na mabadiliko ya tabianchi yaongeza njaa duniani:UM

Baada ya kupungua kwa zaidi ya muongo , zahma ya njaa yaongezeka tena duniani , ikiathiri watu milioni 815  mwaka 2016 , imeonya leo ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa. Patrick Newman na maelezo zaidi

(TAARIFA YA PATRICK)

Ripoto hiyo inayotathimini hali ya uhakika wa chakula na lishe duniani inasema asiliami 11 ya watu wote duniani wameathirika na njaa na wakati huohuo mifumo ya utapia mlo inatishia afya ya mamilioni ya watu ulimwenguni.

Ripori imeongeza kuwa ukilinganisha na mwaka jana kuna ongezeko la watu milioni 38 vichocheo vikiwa ni vita na mabadiliko ya tabia nchi.

Imetaja pia watoto zaidi ya milioni 155 kote duniani walio na umri wa chini ya miaka mitano wana matatizo ya kudumaa na wengine kuwa na uzito mdogo kuliko umri wao. Kostas Stamoulis ni mkurigenzi msaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO idara ya maendeleo na jamii anafafanua sababu

(KOSTAS CUT)

Ripoti imebaini sababu kuu tatu za njaa kuongezeka kwanza kabisa ni ongezeko na ukubwa wa migogoro ambayo imekuwa ikiongezeka kwa muda, sababu ya pili ni hali mbaya ya hewa kama ukame na mafuriko ambayo inaambatana na mabadiliko ya tabia nchi, na sababu ya tatu ni kumekuwa na kudorora kwa uchumi.”

Hii ni ripoti ya kwanza ya Umoja wa Mataifa kutathimini hali ya uhakika wa chakula na lishe kutolewa kufuatia kupitishwa kwa ajenda ya 2030 yenye lengo la kutokomeza njaa na mifumo yote ya utapia mlo kama kipaumbele cha kimataifa.