Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa wa kijinsia ni nguzo muhimu kwa UM: Menéndez

Usawa wa kijinsia ni nguzo muhimu kwa UM: Menéndez

Juma hili Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ametoa muongozo wa kufikia usawa wa kijinsia kwenye Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Ana Maria Menéndez,mshauri wa ngazi ya juu wa Katibu Mkuu kuhusu sera, muongozo huo ameutoa kwa sababu ni moja ya vipaumbele vyake na kwamba

(ANNA CUT 1)

“Mkakati wa usawa wa kijinsia ni muhimu sana sio tu kwa sababu ni haki ya usawa lakini pia nina uhakika utakuwa na athari katika ufanisi na uaminifu wa Umoja wa Mataifa.”

Ameongeza kuwa hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2017 kwa mfano katika mfumo wa Umoja wa Mataifa idadi ya wanawake walio katika kazi za ujuzi katika ngazi ya chini ilikuwa asilimia 50 lakini katika kiwango cha ngazi ya juu cha mamlaka ni asilimia 29 tu, hivyo jinsi ngazi inavyopanda na pengo la usawa linakuwa kubwa zaidi.

Amesisitiza kwamba kwa kulitambua hilo mikakati imewekwa na hatua zinachukuliwa huku Umoja wa Mataifa ukiwa kinara katika kuhakikisha usawa wa kijinsia kuhakikisha unatimia ifikapo 2028 kuziba pengo hilo kwani

(ANNA MARIA CUT 2)

Umoja wa Mataifa pamoja na mambo mengine ni shirika linaloweka viwango, hivyo ni muhimu sana tuwe mfano katika uongozi, na kwamba tutekeleze misingi tunayosuimamia ili tuwahudumie vyema watu wa dunia.”