Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa tuna ‘meno’ ya kudhibiti madawa ya kulevya Tanzania- Dkt. Nyandindi

Sasa tuna ‘meno’ ya kudhibiti madawa ya kulevya Tanzania- Dkt. Nyandindi

Hii leo Umoja wa Mataifa umeadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa ofisi yake inayohusika na udhibiti wa madawa ya kulevya na uhalifu, UNDOC. Ofisi hii kupitia nchi wanachama imechagiza udhibiti wa aina mbalimbali za uhalifu bila kusahau mbinu za kukabiliana na madawa ya kulevya ambayo yanatishia mustakhbali wa wananchi. Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinatekeleza mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kudhibiti madawa ya kulevya ambapo katika kuangazia mwelekeo wa kufanikisha mkakati huo ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, DGS, Assumpta Massoi amezungumza na Kamishna Msaidizi katika mamlaka ya udhibiti wa madawa ya kulevya nchini Tanzania Dkt. Cassian Nyandindi. Dkt Nyandindi pamoja na kuelezea kinachomtia moyo kila uchao na kinachomsikitisha, anaanza kwa kuelezea hatua zilizopigwa na Tanzania kutekeleza makubaliano ya Umoja wa Mataifa.