Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Priyanka ashuhudia jamii zinavyosaidia wakimbizi watoto Jordan

Priyanka ashuhudia jamii zinavyosaidia wakimbizi watoto Jordan

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Priyanka Chopra amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Jordan ambako amekutana na watoto na vijana wa Syria waliosaka hifadhi nchini humo kufuatia vita vinavyoendelea nchini m wao.

Katika ziara hiyo alifika Aman kwenye mradi wa UNICEF uitwao Makani kwa kiarabu au Nafasi yangu ambako jamii za wenyeji wanawasaidia watoto hao.

Alikutana na mtoto aitwaye Warda mwenye umri wa miaka 9 na mdogo wake mwenye umri wa miaka nane aitwaye Ayat.

Watoto hao angalau sasa nuru imerejea kwenye Maisha yao kwa kuwa wameweza kuanza tena shule.

Hawakuweza kusoma kwa miaka miwili kwa sababu familia yao haikuwa na nyaraka za kisheria.

Kupitia vituo hivi, UNICEF na serikali ya Syria wanashawishi uanzishaji wa vituo hivi ili kuwezesha wasichana na wavulna kurejea shule ambapo wanapatiwa stadi za Maisha, kisaikolojia na mafunzo mengine.