Kimbunga Irma chaacha rekodi ya uharibifu

12 Septemba 2017

Tahadhari kuhusu kimbunga Irma iliyotolewa na kituo cha kitaifa cha  hali ya hewa cha Marekani, na kituo cha dhoruba cha kitaifa  kuhusu mafuriko, upepo wa mvua  kalina dhoruba, inaonyesha kuwa Irma  imesababisha uharibifu mkubwa katika maeneo mengi huko Florida.

Kituo hicho kimesema kimbunga Irma tayari kimesababisha  uharibifu katika visiwa vya Caribean  vilivyoko kwenye  usawa wa bahari kama vile Kuba , uharibifu ulitokana na  kimbunga  hicho kuwa katikakiwango chadaraja la 5 .

Wataalamu  hao wamelinganisha  Irma kilichotokea Septemba 10 na kimbunga cha aina kama hiyo cha  mwaka 1924 ,  eneo la Florida Marekani  lieathirika zaidi na  kimbunga hicho kilichiotua kikiwa katika daraja la  4 .

Licha ya  dhoruba hiyo kupungua tarehe 11 septemba bado  hali ni ya kutisha katika maeneo ya kusini mwa Florida  ambapo  thathmini ya madhila ya kimbunga hicho  inategemewa kulingana na ile ya kimbunga harvey kilichotokea kusini mwa Huston Texas.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter