Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu mpya wa OCHA ajionea madhila ya wakimbizi wa ndani Niger

Mkuu mpya wa OCHA ajionea madhila ya wakimbizi wa ndani Niger

Mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA Mark Lowcock yuko ziarani kwenye maeneo ya bonde la ziwa Chad ili kupazia sauti madhila yanayokumba zaidi ya watu milioni 17 kwenye eneo hilo.

Mathalani tayari ametembelea kambi ya wakimbizi wa ndani ya N’Gagam kusini-mashariki mwa Niger ambako amekutana na wanawake na wanaume waliomweleza madhila wanayopitia na kuahidi kuwasilisha wakati wa mjadala mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoanza wiki ijayo.

Tangu mwaka 2015, maeneo ya kusini-mashariki mwa Niger yamekuwa yakikumbwa na mgogoro kutokana na mashambulizi ya Boko Haram ambayo yamesababisha maelfu ya raia kulazimika kukimbia .

Karibu watu 250,000 wamekimbia  makazi yao katika jimbo la Diffa, wengi wao wanaishi na familia za wenyeji huku 400,000 katika jimbo hilo wakiwa katika hali ya sintofahamu.