Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo na uharibifu wa tetemeko la ardhi Mexico umenishtua:Guterres

Idadi ya vifo na uharibifu wa tetemeko la ardhi Mexico umenishtua:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na idadi ya vifo na uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi la mwishoni mwa juma kwenye majimbo ya Oaxaca, Chiapas na Tanasco nchini Mexico na kusema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada endapo utahitajika.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Mexico, huku akiwatakia ahuweni ya haraka majeruhi.

Ameipongeza serikali na wahudumu wa dharura kwa juhudi zao za kuwasaidia wanaohitaji msaada na kuhakikisha wanarejesha huduma za muhimu katika jamii.

Katibu Mkuu pia amewahakikishia watuna serikali ya Mexico kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia endapo utahitajika.