Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto 1 kati ya 5 wanahitaji msaada Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini:UNICEF

Mtoto 1 kati ya 5 wanahitaji msaada Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini:UNICEF

Karibu mtoto mmoja kati ya watano Mashariki ya Kati na Afrika ya Kasakazini wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kwa mujibu wa takwimu na uchambuzi wa karibuni wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Patrick Newman na taarifa kamili

(TAARIFA YA PATRICK)

Takwimu hizo zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimi 90 ya watoto hao wanaishi kwenye nchi zilizoathirika na mizozo. Vita vimeendelea kuwapokonya mamilioni ya wasichana na wavulana utoto wao, huku miongo ya hatua zilizopigwa katika nchi hizo ikiwa hatarini amesema Geert Cappelaere mkurugenzi wa kikanda wa UNICEF.

UNICEF imetaja baadhi ya athari zinazowakabili watoto hao kuwa ni pamoja na kutawanywa na kukosa huduma za msingi za binadamu . Miundombinu ya kijamii ikiwemo hospitali, nishati, shule mitambo ya maji na huduma za kujisafi mara kadhaa vimeshambuliwa na kuwaweka watoto hao katika hatari kubwa ya vifo na magonjwa.

Ameongeza kuwa kukiwa hakuna dalili yoyote ya kumalizika kwa vita ,familia nyingi hazina chaguo isopokuwa kuwatoa watoto wao kufanya kazi au kuingia kwenye ndoa za utotoni.

Takribani watoto milioni 12 ni waathirika Syria na milioni 2 kati yao wako katika maeneo ambayo ni vigumu kuyafikia.