Baraza Kuu lajadili utamaduni wa amani #CultureOfPeace

7 Septemba 2017

Hii leo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeakuwa na kikao cha ngazi ya juu kikiangazia utamaduni wa amani, jambo ambalo linaelezwa kuwa hivi sasa linafifia.

Akizungumza kwenye mkutano huo mshauri mwandamizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera Ana María Menéndez amesema mizozo inaongezeka kila uchao katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, sambamba na wigo wa madhara yake.

Amesema mizozo hiyo inasababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kuzuia fursa za binadamu kuchanua pamoja na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Amemnukuu wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka raia wote, serikali zao na viongozi kuweka pembeni tofauti zao na kuazimia kupatia amani kipaumbele.

Na zaidi ya yote ili amani iweze kuwa utamaduni wa kila mtu Bi. Menéndez amependekeza mambo manne ikiwemo..

“Mosi uwekeze kwa watoto tangu elimu ya utotoni ili kuondoa fikra potofu za wao na sisi. Pili tuwekeze kwa vijana kwani hakuna kundi moja la kijamii ambalo ni muhimu duniani kwa kujenga amani kama vijana wa kike na kiume. Tatu, tunapaswa kutambua kuwa mchango wa wanawake kwenye amani ni muhimu. “

Pendekezo la nne ni kuwekeza katika ujumuishaji wa jamii kiuchumi, kisiasa na kijamii akisema kuwa ni muhimu kwa kuwa ni lazima kutambua tofauti baina ya watu ni fursa na si kitisho.

Naye Rais wa Baraza Kuu Peter Thomson amesema..

(Sauti ya Thomson)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter