IOM yazindua wavuti mpya kufuatilia wahamiaji
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limezindua wavuti mpya kwa ajili ya wahamiaji ambao hawajulikani waliko.
Mradi huo utafuatilia wahamiaji ikiwemo wakimbizi na waomba hifadhi ambao wamefariki dunia au ambao wametoweka wakati wakielekea katika nchi ya kigeni.
Wavuti huo ambao umekarabatiwa upya unajumuisha jedwali jipya na ramani ambazo zitawezesha mtu kufuatilia takwimu kwa mwezi, mwaka au eneo.
Aidha inajumuisha kurasa zaidi kwa ajili ya kufuatilia maeneo hatarishi kwa mfano Mediterenea na Mashariki ya kati.
Halikadhalika mradi utaonyesha takwimu kwa kina na kwa undani zaidi.