Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yapendekeza mbinu za kudhibiti habari za uongo

UNESCO yapendekeza mbinu za kudhibiti habari za uongo

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limetoa mapendekezo 15 yenye lengo la kukabiliana na habari bandia au za uongo ambazo hivi zimeshamiri kwenye mitandao ya kijamii.

Guy Berger ambaye ni Mkurugenzi wa UNESCO wa masuala ya uhuru wa kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari amewasilisha mapendekezo hayo mbele ya wabunge wa bunge la Muungano wa Ulaya.

Mapendekezo hayo ni pamoja na vyombo vya  habari kuimarisha mafunzo ya watendaji wake ili kujenga uwezo wa kufahamu habari za ukweli pamoja na kuepusha wavuti ambazo zina matangazo yanayobeba habari za uongo.

Halikadhalika Bwana Berger amependekeza waandishi wa habari wawe mstari wa mbele kubaini na kuweka hadharani habari za uongo akisema kuwa wanaosambaza habari hizo lengo lao ni kuondoa uhalali wa vyombo vya habari vinavyozingatia ueledi.

Katika mkutano huo ulioandaliwa na bunge hilo la EU, Berger pia ametaka

serikali zichukue hatua kulinda waandishi wa habari huku ikiwashtaki wale wanaoeneza habari za uongo.