Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yasaidia wanaokimbia ukatili Myanmar

WFP yasaidia wanaokimbia ukatili Myanmar

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linapatia msaada watu waliokimbilia Bangladesh kufuatia vitendo vya ukatili vinavyofanyika jimbo la Rakhine nchini Myanmar.

Tayari WFP imetoa msaada kwa zaidi ya watu 28,800 kwenye wilaya ya Cox's Bazaar mpakani na Myanmar ambapo wamepatiwa vyakula kama vile biskuti zilizorutubishwa, wali na mbaazi.

WFP inasikitishwa na hali ya kiafya ya wanawake na watoto wanaowasili wakiwa na njaa na utapiamlo ambapo shirka hilo linawapatia uji wa lishe bora uliotengenezwa kwa unga wa ngano na soya.

Takriban watu 146,000 wamemiminika kwenye mpaka na kuingia katika wilaya hiyo ya Cox’s Bazar tangu Agosti 25 wakitafuta hifadhi wengi wao wakiwa ni wanawake, watoto na wazee.

WFP imeimarisha juhudi zake kuwasaidia na imetolea wito wahisani kuwasadia ili waendeleza shughuli za msaada wa kibinadamu