Guterres asikitishwa na madhara kufuatia mafuriko nchini Bangladesh, India na Nepal

Guterres asikitishwa na madhara kufuatia mafuriko nchini Bangladesh, India na Nepal

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres ameelezea kusikitishwa kwake na vifo na madhila wanayokumbana nayo watu nchini Bangladesh, India na Nepal kufuatia mvua kali zilizosababisha mafuriko.

Guterres kupitia taarifa ya msemaji wake ametuma salamu za rambi rambi kwa serikali na watu wa Bangladesh, India na Nepal na kupongeza serikali hizo kwa uongozi katika kukabiliana na mahitaji ya waathirika.

Amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada wa kibinadamu.