Somalia yaweza kuinua ustawi wa wakimbizi wa ndani: Kalin

Somalia yaweza kuinua ustawi wa wakimbizi wa ndani: Kalin

Mshauri mwandamwizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukimbizi wa ndani Walter Kalin amesema Somalia yaweza kuanzisha mfumo bora na pia ufumbuzi wa kudumu nchini kwa kushirikiana na uongozi wa serikali, ambao utahamasisha zoezi la upatikanaji fedha za kusaidia kuinua  viwango vya maisha ya  wakimbizi wa ndani.

Akiwa katika ziara ya juma moja nchini Somalia Bwana Kalin amesema kile kilichomfikisha Jubbaland.

(Sauti ya Kalin)

"Nimekuja hapa kushudia maendeleo yaliyotolewa na serikali ya Jubbaland. Imewapa ardhi wakimbizi wadani waliorudi, hi inatia moyo sana. Lakini tunahitaji kuwekeza zaidi katika maendeleo ya maeneo haya kwa kuinua uchumi wa  mji wa Kismaayo, watu hawa waweze ili watu waweze kunufaika kiuchumi”

Ikiwa  ni mara yake ya tatu nchini Somalia Bw. Kalin alipata fursa  ya kutembea miji kama Kismaayo, mji mkuu wa Jubaaland, Dollow na mji wa Geddo mpakani na Ethiopia.

Pia alikutana na makamu wa kwanza wa rais Mohamud Sayid Aden kuzungumzia suluhisho la migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na  wakimbizi wa ndani.