Shairi ‘Head over heels’ latoa taswira ya madhila ya wakimbizi wa Sudan Kusini

Shairi ‘Head over heels’ latoa taswira ya madhila ya wakimbizi wa Sudan Kusini

Takriban wakimbizi milioni moja wa Sudan Kusini wamekimbilia nchi jirani ya Uganda, hii ikiwa ni nchi inayowahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Sudan Kusini. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya kusaidia wakimbizi hao wa Sudan Kusini na serikali ya Uganda inayowahifadhi.

Mbinu mbali mbali zinatumika kupaza sauti ya madhila wanayokumbana nayo wakimbizi kutoka Sudan Kusini na kwingineko ambapo katika makala hii Grace Kaneiya ameangazia shairi ‘Head over heels’ la Emi Mahmoud mzaliwa wa Darfur, Sudan ambaye anaishi Marekani, ungana naye.