Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya maji ikihitimishwa, watoto waeleza ukosefu wa maji unavyowaathiri kielimu

Wiki ya maji ikihitimishwa, watoto waeleza ukosefu wa maji unavyowaathiri kielimu

Wiki ya maji duniani ikihitimishwa leo, Umoja wa Mataifa unasema suala la maji na huduma za kujisafi ni muhimu katika kutekeleza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu, SDGs. Patrick Newman na tarifa kamili.

(TAARIFAYA PATRICK)

Maudhui ya wiki ya maji mwaka huu ni "Maji na taka: Punguza na tumia tena" kauli inayochagiza uhifadhi wa maji na matumizi sahihim sanjari na lengo namba sita la SDGs.

Nchini Tanzania mtandao wa watoto wanahabari wa mkoani Mwanza,  unaoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, umeangazia wiki hii kwa kuzungumza na wanafunzi ambao wanaeleza adha ya ukosefu wa maji na atahri zake katika masomo.

(Sauti za Wanafunzi)

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha takribani watu bilioni 2.4 hawana huduma za kujisafi huku idadi kubwa ya wati kwenye kanda na  nchi wanakabiliana na uhaba wa maji unaochagizwa na kuongezeka kwa idadi ya watu, kukua kwa miji na pia mabadiliko ya tabianchi.