Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu akaribisha hatua ya kuachiwa huru viongozi Cameroon

Katibu Mkuu akaribisha hatua ya kuachiwa huru viongozi Cameroon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekaribisha kuachiwa huru kwa baadhi ya viongozi wa Cameroon kutoka maeneo ya Kusini Magharibi na Kaskazini Magharibi na kutupiliwa mbali kwa mashataka dhidi yao Agosti 30 baada ya amri ya rais Paul Biya.

Kupitia taarifa ya msemaji wake, Guterres ana matumaini kwamba hatua hii itapelekea katika kupunguza mvutano na kuimarisha majadiliano.

Katibu Mkuu amehimiza mamlaka Cameroon kuendeleza juhudi za kukabiliana na malalamiko ya jamii ili kupata suluhu ya kudumu kwa mzozo.

Guterres amesisitiza u tayari wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono juhudi za upatanishi.