Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid ataka hatua zichukuliwe dhidi ya Venezuela

Zeid ataka hatua zichukuliwe dhidi ya Venezuela

Uhuru wa kujieleza unabanwa nchini Marekani na hili lina madhara. Hii ni kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Zeid Ra'ad Al Hussein wakati akihutubia waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi kuhusu hali inyaoendelea kuzorota nchini Venezuela. Katika mkutano huo kuhusu Venezuela, aliulizwa swali kuhusu matamshi dhidi ya waandishi wa habari nchini Marekani, Zeid amesema

(Sauti ya Zeid)

“Kongamano kubwa ambalo linataja waandishi wa habari kama watu wabaya mno, sio lazima mtu kutafakari sana kuelewa ni lipi linaweza kutokea, na ninaamini kwamba kuna mwandishi wa habari kutoka gazeti la Guardian ambaye alishambuliwa hivi maajuzi nchini Marekani, na hili ni jambo la kusikitisha kwamba iwapo inafanyika Marekani basi unajiuliza ni yapi yatafanyika kwingineko ambako mchango wa waandishi wa habari kwenye jamii hautiliwi maanani.”

Kuhusu Venezuela, amesema kumekuwa na wimbi la ukandamizwaji wa haki tangu kuchaguliwa kwa Rais Nicolas Maduro na amependekeza hatua zichukuliwe.

(Sauti ya Zeid)

Kwa hiyo nitahimza Baraza la haki za binadamu kuchukua hatua kuhakikisha hali ya kibindamu nchini Venezuela, ambayo ni mwanachama haiendelei kuzorota.”